MASHADA INC

Friday, December 21, 2012

EXCLUSIVE; LEMA ASHINDA RUFAA, ARUDISHWA KUWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI

Godbless Lema akishangilia mara baada ya haki kutendeka
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema leo ameshinda rufaa ya kesi yake.
Mahakama imejiridhisha kuwa madai ya udharirishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji (CCM). Tangu sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema. CCM wameamriwa kulipa gharama za kesi hii tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia!

Nukuu kutoka kwa Neville Meena (akiwaandikia Wanamabadiliko Tanzania):

Kweli Karejeshewa Ubunge kwa hoja kubwa moja.
Walioshtaki hawana haki ya kufanya hivyo kwa kuzingatia aina ya hoja walizowasilisha. Matusi dhidi ya Burian hayawahusu wao, alipaswa kulalamika mwenyewe.

Kutoka kwenye blogu ya Libeneke la Kaskzaini, “FURAHA ZATANDA KATIKA MITAA YA JIJI LA ARUSHA KUFUATIA LEMA KUREJESHEWA UBUNGE” 

Mama huyu anashangilia ushindi wa Lema leo
Wanachi wa mkoa wa Arusha leo wamebujikwa na furahaa mara baada ya kusikia kuwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini amerudishiwa ubunge wake.

Wakiongea wakiwa na furaha kwa nyakati tofauti wamedai kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuweza kuwasimamia na kuweza kumuongoza Jaji kufanya maamuzi mazuri kwa kufuata sheria bila ya kushawishiwa na mtu yeyote.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Omari Ally alisema kuwa Godbless Lema anastaili kupewa Ubunge wake kwakuwa alichaguliwa na wananchi wake na sio alitumia njia za uchochoroni.

Naye mwananchi mwingine alisema, “Unajua kuwa kweli walimuaonea Lema sana kwani alikuwa na anastaili kuwa Mbunge wetu, kwani tulimchagua wenyewe; Na katika Wabunge ambao walichaguliwa na kupita kwa kishindo kikubwa ukiangalia mkoa wa Arusha ni mbunge huyu wa Arusha Mjini pamoja na mbunge wa jimbo la Arumeru, hivyo jamani Mungu katenda miujiza kweli tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu,” alisema Mathayo Mushi

Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Neema Raphaeli alisema kuwa yeye anapenda kumuomba Mbunge huyu kuanza kazi kwa kuwatetea wamama ambao wanauza mboga pamoja na nyanya na matunda wakiwa wamebeba katika makarai yao kwani wamekuwa wananyanyaswa sana kwa kunyanganywa vitu vyao, hivyo alimuomba mbunge lema kuanza na kuwatetea wao kwani wameteseka kwa muda mrefu.

Wamachinga mbalimbali walikuwa wameweka vitu vyao barabarani wakifurahia kwa shangwe huku wakibainisha kuwa mtetezi waoamekuja na kwa sasa watafanya biashara bila ya kubugudhiwa na mtu yeyote, kwani kuwa atawatetea.

“Kwa kweli tunafuraha ambayo hatuwezi kuelezea mtetezi wetu amekuja bwana na uhakikia izishida za kufukuzwa zitaisha na kweli sasa ivi mgambo yeyote aote kuja kutunyanganya kitu au amnyanganye mama yeyote atatutambua” walisema wamachinga hao.

Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...