MASHADA INC

Tuesday, December 11, 2012

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI NA KUPEWA MILLIONI 10 - AHAIDIWA NYINGENE MWISHO WA MSIMU

Mrisho Ngassa akisalimiana na Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji wakati wa kombe la Kagame
Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.

Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.

"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."

Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000.

Souce;www.shaffihdauda.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...