MASHADA INC

Thursday, December 13, 2012

KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY (KIU) WAPO KWENYE MGOMO

Wanachuo wa chuo wa kampala university wako kwenye mgomo kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutatua matatizo yao. Aidha wanachuo hao ambao kwa siku kadhaa zimepita walikaa kikao na uongozi wa chuo hicho lakini kikao hicho hakikuweza kufikia makubaliano, sasa wanachuo hao wameamua kugoma ili kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutatua matatizo yao. Madai ya wanafunzi hao ni ulipaji wa ada ambapo chuo hicho hakifuati mfumo wa TCU unavyosema kwenye vitabu vya TCU ulipaji wa ada ni kwa kutumia fedha ya kitanzania lakini chuo hicho unalipa ada kwa mfumo wa dolla.

Wanafunzi hao wanapinga ulipaji wa dolla kwa madai unawaumiza wao hii ni kutokana na ubadilisha wa dolla aidha wanadai kuwa chuo hicho hakina prospectus book yani kitabu kinacho onesha mfumo wote wa chuo unafanyeje kazi ikiwepo na kozi wanazofundisha. Hii imekuwa tabu kwao, pia wanadai kuwa Faculty za Health Science hazina maabara za kutosheleza wanafunzi wote. Wanafunzi hao waliokuwa wakiongea kwa uchungu walisema walikuwa kila siku wanaongea na uongozi wa chuo hicho kuhusiana na matatizo yao lakini uongozi wa chuo hicho hauyafanyii kazi.

Aidha baadhi ya watu kutoka TCU walifika chuoni hapo kuongea na uongozi wa chuo hicho iliwafuate mfumo wa TCU lakini uongozi huu ulitoa majibu ya mdomo wakati wanafunzi wa chuo hicho wanataka majibu yawe kimaandishi. Hadi kufikia jana mkuu wa chuo hicho hakusaini nyaraka ambazo zina mtaka kufuata utaratibu wa TCU katika ulipaji wa ada tulijaribu kuwatafuta viongozi wa wanafunzi lakini hatukufanikiwa. Wanafunzi hao wamesema kuwa uongozi wa chuo hicho hauwajali maana wanapoteza muda wao wote wa masomo wakati muda huu wangekuwa darasani wanasoma badala yake hawasomi kutokana na matatizo. Kiukweli Mtanzani hawezi kulipa ada kwa dolla hii kwasababu kwanza yupo nchini kwake nilazima atumie fedha ya nchini kwake kuliko kutumia fedha za kigeni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...