MASHADA INC

Tuesday, December 11, 2012

EXCLUSIVE; MBEYA ALL STARS KUJA NA "SALAMU KUTOKA MBEYA"

Baada ya kusumbua kwa muda mrefu na ngoma yao ya Mbeya nyumbani, Wasanii wakali kutoka jijini Mbeya hapa nawazungumzia Mbeya All Stars wanakuja na pini jipyaaaaaaa linalokwenda kwa jina la Salam toka Mbeya. Akiongea na mhariri wa UJIO WANGU vice president wa Mbeya All Stars Doctor Fazi amesema "Ngoma hiyo inatarajiwa kuachiwa rasmi kesho tar 13/12/2012"

Akizungumzia ngoma hiyo producer wa ngoma hiyo Zest Mkali kutoka Moja Moja records amesema kwamba kutakua na wasanii wapya ambao hawakushiriki kwenye nyimbo zilizopita hii ni kuonyesha kuwa dhamira ya Mbeya All Stars ni kuinua vipaji na kuvitangaza kuanzia nyumbani.
Pia vice president wa Mbeya All Stars ameongeza kua hivi karibuni kutakua na ujio wa blog mpya itakayoitwa THE GREEN CITY PROFILE itakayokua ikizungumzia ma-celebrity wa jiji la Mbeya kwa kuweka picha zao na CV zao.
Stay tuned mambo mazuri Kutoka MBEYA ALL STARS yanakuja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...