Saturday, February 2, 2013

BREAKING NEWS; PPF TOWER{Dar es salaam} INAUNGUA MOTO MDA HUU


PPF Tower inawaka moto muda huu, Jengo hilo ambalo lipo makutano ya Mtaa wa Ohio na Garden Avenue linawaka moto mkali juu kabisa, fire zimefika na jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea ingawa imekuwa vigumu sana kufanikiwa kutokana na urefu wa jengo ni vitendea kazi wanashindwa kupanda.

Endelea kutembelea blog hii tutaendelea kukujuza kinachoendelea.

UPDATES;
Taarifa zinasema kuwa,hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo juu, mwisho kabisa mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha moto asubuhi ya leo majira ya saa moja, na kusababisha jengo hilo ushika moto.

Imetaarifiwa kuwa walinzi wa jengo hilo walishuhudia moshi mzito ukitoka ndani ya jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.

Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi ghorofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo.
Hata na hivyo, juhudi zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo kabisa mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.

Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.

Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...