Sunday, February 10, 2013

YOUNG RAFA; DOGO JANJA SI LOLOTE KWANGU, HATA YEYE ANAJUA HILO

Young Rafa
Rapa YOUNG RAFA(16) kutoka jijini Rock City(Mwanza) aliye chini ya Record label ya THE EMPIRE,  ameibuka na kusema kuwa kipaji chake cha ku-rap hakifananishwi na yeyote na kudai kuwa wanaodhani Msanii Dogo Janja{Janjaro} aliyekua kundi la Tip Top Connection kabla ya kufukuzwa na sasa yuko chini ya Mtanashati ni tishio kwenye mziki anaofanya basi wamepotea kama Janjaro anavyopotea.

Akizungumza na UJIO WANGU BLOG, Young Rafa amesema "Dogo Janja si lolote kwangu na hana uwezo wa kushindana na mimi kwa namna yoyote" aliendelea kuongeza kuwa "Dogo Janja hana anachokifanya kwenye gemu zaidi za kujisifia, fuatilia nyimbo zake utaona hilo, Mimi{Young Rafa} naandika mashairi yenye maana na ujumbe kwa jamii, mfano nyimbo yangu ya MAMA DON'T CRY ni nazungumzia matatizo mbalimbali wanayokutana nayo mama zetu katika maisha ya kila siku".
Young Rafa akiwa na  Baba Levo
Aliongeza na kusema "Dogo Janja anabahati tu alipata watu wa kumsimamia ambao tayari wana-influence kubwa kwenye muziki wa bongo na ndio maana alitangulia kutoka. Kama sio pesa uwezo wake sio wa kunitangulia kutoka."

Young Rafa alimaliza kwa kusema "nachoweza kumuahidi ni kwamba asubiri kuona wasanii wa ukweli tunavyofanya kazi. Na kama akitaka kubaki kwenye game basi ajifunzie uandishi kwangu na aanze kuandika vitu vya maana"

Jina kamili la rapa huyo ni RAPHAEL CHARLES na umri wake ni miaka 16. Kwa sasa dogo huyo anasoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Mkuyuni iliyoko Maina, jijini Mwanza. Hizi hapa ni baadhi ya nyimbo zake alizorekodi katika studio za RAV MEDIA chini ya producer Mnyambudu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...