Thursday, May 16, 2013

TAZAMA VIDEO INAYOONYESHA JINSI FRANCIS CHEKA ALIVYOONEWA HUKO UJERUMANI(F CHEKA vs UENSAL ARIk)Wiki kadhaa zilizopita bondia anayetikisa Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki Francis Cheka alikaririwa na kituo kimoja cha redio akilalamikia maamuzi mabaya katika mpambano wake wa kimataifa  dhidi bondia kutoka ujerumani Uensal Arik ikionekena dhahiri mjerumani huyo kununua mchezo kutoka kwa promota aliyeandaa mpambano huo.Video hapo juu inaonyesha jinsi promota huyo ambaye wakati wote wa mpambano ndiye alikuwa msaidizi wa Cheka na ndiye alivunja mpambano katika round ya 6 baada ya kurusha kitambaa (taulo) ikiashiria bondia Cheka kazidiwa katika round hiyo wakati sio kweli kwamba Cheka alikuwa ameshinda. Akiongea na UJIO WANGU kwa njia ya simu bondia Francis Cheka anasema promota huyo alimfuata hotelini alipofikia na kumwambia akubali kuuza mpambano huo lakini Cheka alikataa na hakuwa tayari kuuza.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...