Kitu kikubwa kilichonifanya nishindwe kuvumilia hili ni kwamba jambo hili linafahamika na liko wazi kwa kila mwananchi na serikali kiujumla na ukiwakuta akina dada hao wakifanya ufuska huo wanao uita BIASHARA, utawaona wako huru na wanaojiamini kama vile wanachokifanya ni halali na wanastahili kukifanya!
Katika harakati za kutaka kujua zaidi nilifanya mahojiano na baadhi ya akina dada hao(makahaba) kutaka kujua kipato chao katika ufuska wao wanaouita biashara, wengi wao walisema biashara ni nzuri na kwa wastani wanapata kati ya elfu ishilini(20,000) hadi elfu arobaini(40,000) kwa siku. Hii ndio sababu kubwa ilionifanya nijiulize NI NANI AWATOZE KODI AKINA DADA WANAOJIUZA? kwani kipato chao ni kikubwa zaidi ya wafanyabiashara wa kawaida!
Hoja ya msingi ni kwamba maeneo yote wanayofanyia ufuska huo akina dada hao yanafahamika wazi na serikali na hakuna juhudi zozote zinazofanyika kuonyesha kupinga suala hili na kama halipingwi tafsiri yake ni kwamba ni halali kufanya ukahaba na kama ndivyo basi walipe kodi, suala ni nani awatoze kodi?
No comments:
Post a Comment