Wapiganaji wa Yanga wakiteta kabla ya kuzungumza na wachezaji leo
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akiwaeleza jambo viongozi wenzake wa YangaManji, Sanga, Katabalo na Bin Kleb wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na wachezaji
Manji akiondoka klabuni kwa gari lake binafsi baada ya kuzungumza na wachezaji
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji leo ametembelea tena makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kuzungumza na wachezaji. Manji alifika klabuni hapo akiwa ameongozana na makamu wake, Clement Sanga, wajumbe wa kamati ya utendaji, Abdalla Bin Kleb na Mussa Katabalo pamoja na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili, Seif Ahmed. Viongozi hao walikutana na wachezaji kwa saa kadhaa na kuzungumza nao mambo mbalimbali kwa lengo la kuwaweka sawa kabla ya mechi yao ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar. Yanga inatarajiwa kushuka dimbani leo kucheza na Mafunzo katika mechi ya pili ya robo fainali itakayoanza saa 10 jioni. Katika mechi ya awali, URA ya Uganda itavaana na APR ya Rwanda. Katika kikao hicho cha faragha, inasemekana kuwa Manji na viongozi wenzake waliwataka wachezaji kutambua vyema jukumu lililo mbele yao na kuongeza jitihada ili waweze kufika mbali zaidi. Alisema mechi hiyo ni muhimu kwao kwa vile iwapo wataishinda Mafunzo watafuzu kucheza nusu fainali na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa.
SOURCE;http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment