OKWI |
Katibu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba, Okwi ambaye tayari yuko huko kwa wiki moja, hadi sasa anafanya vizuri ndio maana kapewa wiki mbili zaidi, ili kocha wa klabu hiyo ajiridhishe zaidi na kiwango cha Mganda huyo.
Klabu hiyo inayotumia Uwanja wa Red Bull Arena, ikiwa zaidi inafahamika kama SV Austria Salzburg kabla haijanunuliwa na kampuni ya Red Bull mwaka 2005, imewahi kufika Fainali ya Kombe la UEFA mwaka 1994 na inacheza Ligi Kuu ya Austria, iitwayo Bundesliga kama Ligi Kuu ya Ujerumani.
Timu hiyo ni kama timu ambayo Okwi, anachezea kwa sasa, Simba SC, kwani nayo inavaa jezi za rangi ya nyeupe na nyekundu na imewahi kutwaa taji la Bundesliga ya Austria mara saba na pia ilicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1994–1995 kama Casino Salzburg, na kuwa timu pekee, ambayo haikufungwa na mabingwa wa wakati huo, Ajax Amsterdam.
Awali, Okwi aliikosesha Simba Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya
Afrika Kusini na kuamua kwenda Austria, ambako inaelezwa klabu hiyo iko tayari kutoa Euro 600,000
akifuzu.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma. Hata hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu.
Wakala aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL).
No comments:
Post a Comment