Kwa kipindi kirefu kidogo toka mwaka 2012 kumekua na taarifa mbalimbali zinazopita kwenye magazeti, blogs na midomoni mwa watu kadhaa kwamba staa wa muziki wa bongofleva anaetajwa kulipwa pesa kubwa kwenye kufanya show Tanzania Diamond Platnums ameshuka kiwango, yani mwisho wake kwenye muziki umefika.
Baada ya hizo taarifa nimekua nikijaribu kufanya interview na Diamond lakini hakupenda kuliongelea hilo kwa wakati huo. Diamond amebadili huo msimamo na kuamua kufunguka rasmi kwenye Exclusive interview na millardayo kuhusu yote yanayosemwa kwamba kashuka kiwango.
Namkariri akisema “unapofanya vizuri hakuna anaependa, kama Maisha Club wasanii wengi huwa wanafanya show lakini nikifanya mimi ndio panatapika hata club nyingi hata nilivyofanya show Dar Live uliona watu kutaka kutia virusi, kutaka kutengenezea mazingira”
“Mashabiki ndio wanatakiwa kusema flani labda sasa hivi ameshuka lakini mashabiki hao ndio hao kila siku wanazidi kununua kazi zangu, wanazidi kuomba nyimbo zangu kwenye redio.. kiukweli nyimbo zangu ndio zinaombwa sana kwenye radio, katika show zangu wanajaa sana” – Diamond
Kwenye sentensi nyingine Diamond amesema “kuna gazeti likaandika Diamond sijui ndio mwaka wake wa mwisho, Diamond sijui ameshuka kiwango… utaweza vipi kuandika vitu kama hivyo? mi ndio msanii ambae nalipwa pesa nyingi kuliko msanii mwingine yoyote Tanzania, vita za kibiashara kokote zipo mimi ndio maana hazinishtui kila siku ndio maana nazidi kuachia ngoma tu kuwakata vilimi vilimi, wanatakiwa wajue kabisa kwamba mimi nimeaga nyumbani… licha ya kuaga mi nafanya muziki kama kazi kwa njaa kabisa, kwa hiyo mwenyezi Mungu alienipandisha na mashabiki zangu ndio wanaweza wakataka kunishusha”
HII NI MOJA YA TWEET YA PROFESOR J, AKIMZUNGUMZIA DIAMOND;
“Mashabiki ndio wanatakiwa kusema flani labda sasa hivi ameshuka lakini mashabiki hao ndio hao kila siku wanazidi kununua kazi zangu, wanazidi kuomba nyimbo zangu kwenye redio.. kiukweli nyimbo zangu ndio zinaombwa sana kwenye radio, katika show zangu wanajaa sana” – Diamond
HII NI MOJA YA TWEET YA PROFESOR J, AKIMZUNGUMZIA DIAMOND;
No comments:
Post a Comment