Saturday, December 24, 2011

BEST QUOTE 2011/ NUKUU BORA MWAKA 2011

                                      MH;Godbless Lema, Mb (Arusha Mjini)

“Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu, katika mazingira haya nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine.
“Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi, tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi''.
Nilioona mabinti wadogo wakifanya biashara ya ukahaba, nilitafakari kisha nikatafakari tena, dhahabu, almasi, milima na mabonde, tanzanite, samaki, ureniamu, makaa ya mawe, utalii, ardhi na kilimo na zaidi utu na mahusiano mazuri nikaona siwezi kukaa kimya tena lazima nitoe sauti isikike.
Ni heri vita inayotafuta haki, usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu na kwamba katika msingi huo hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu na simwogopa mtu yeyote mwenye silaha, mwenye cheo chohote na wala sitaogopa jela yoyote ilihali nanapigania haki na utu.
“Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendelea kutunyanyasa bila sababu ya msingi''.
"Sisi tunajua tutashinda kwa sababu haki tunayoipigania ni makusudi ya Mwenyezi Mungu, leo nitaenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa nia ya kujitafutia utukufu,”.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...