Friday, December 23, 2011

YOUNG DEE: BIRTHDAY NA MAJONZI.

YOUNG DEE
Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini anaetamba na wimbo wake ujulikanao kama Tunapeta siku ya leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa, Akizungumza na kituo kimoja cha radio hapa nchini rapa huyo amesema kuwa anamajonzi makubwa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kutokana na maafa makubwa yaliyo tokana na mafuriko sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam na kwingineko nchini.
Akizungumzia kuguswa kwake Young Dee amesema kuwa yeye kama mwanajamii anajitolea 60% ya kipato chake atakachopata katika show ya Step-up player itakayofanyika kesho tarehe 24. Young Dee amezidi kuwaomba watanzania kujitolea kwa hali na mali kwani tatizo hili ni la kitaifa na kusema kutoa ni moyo sio utajiri.
Mbali na Young Dee, wanamuziki mbali mbali wanaendelea kujitokeza kuwasaidia wahanga kwa namna mbali mbali wakiwemo TMK wanaume Family ambao pia wameahidi kuchangia kutokana na mapato watakayopata katika show zao na weekend hii.
WATANZANIA TUJITOLEE KWA KILE TUNACHOWEZA, TANZANIA PAMOJA HULETA PAMBAZUKO JIPYA.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...