MASHADA INC

Monday, March 26, 2012

MESI KAMA BOKO


John Boko"Adebayo" wa timu ya soka ya Azam Fc ya jijini Dar es salaam anaongoza kwa ufungaji katika ligi kuu ya Tanzania bara akiwa na magoli 15 akichangia kwa kiasi kikubwa timu yake kushika nafasi ya pili mpaka sasa katika msimamo wa ligi hiyo. Boko amekua akifanya vizuri sana katika timu yake lakini anaonekana kuboronga katika timu ya taifa"Taifa Stars" ambako hukosa magoli mengi ya wazi kiasi kwamba mashabiki huishia kumzomea..

Vivyo hivyo kwa Lionel Mesi m'argentina anaekitimua katika timu kubwa duniani Fc Barcelona ya nchini hispania amekua mwiba mkali kwa kila timu pinzani anapokua Barcelona, mpaka sasa anaongoza kwa kuzifumania nyavu akiwa na magoli 34 na kuisaidia timu yake kukamata nafasi ya pili lakini amekua akilaumiwa na wadau mbalimbali wa soka duniani kwani anapokua katika timu ya taifa ni kama Boko msaada wake hauonekani. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...