MASHADA INC

Wednesday, October 24, 2012

CHUJI AZICHAPA NA SHABIKI BAADA YA KUIFUNGA POLISI MORO

ATHUMAN IDD CHUJI amefanya kitendo cha aibu baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Yanga na Polisi morogoro, Chuji aliamua kuanza kumpiga mshabiki wa Yanga nje ya uwanja, tukio hilo la aibu lilianza mara baada ya mshabiki kuwaambia wachezaji wamecheza chini ya kiwango japo Yanga ilishinda, shabiki huyo ambaye ni mmoja kati ya mashabiki maarufu wa Yanga aliendelea kuwaambia wachezaji waongeze bidii kwani wanalipwa pesa nyingi.

Chuji aliyekuwa ameambatana na Nurdin Bakari kuelekea kwenye basi la Yanga lililokuwa limesimama nje ya uwanja wa Taifa alianza ghafla kumkimbiza huku akimrushia mateke na ngumi shabiki huyo, Nurdin Bakari pamoja na mashabiki wengine walikua wakimfuata na kumsihi aache kumpiga shabiki huyo.

Mashabiki wengi walichukizwa na kitendo kile na kuonyesha kutopendezwa na mwenendo wa mchezaji huyo huku wengi wakidai ameshuka kiwango na walijiuliza yeye nani mpaka asiambiwe ukweli? Mashabiki hao waliendelea kukaa nnje ya uwanja wa Taifa wakiwasubiri wachezaji na kuwaambia ukweli wenyewe wanaita makavu.

Saimon Msuva ni mmoja kati ya wachezaji walioitwa na mashabiki na kuambiwa ukweli, wengi walimsihi apunguze unyimi wa pasi uwanjani na asijione staa, PIA mashabiki waliwasubiri viongozi wa yanga waliokua wakiongozwa na Bin Kleb na kuwaeleza kutoridhishwa na mwenendo na tabia za wachezaji, Bin Kleb aliahidi kuyafanyia kazi na kuongea na wachezaji juu ya yote waliyoongea mashabiki.

Saimon Msuva akishangilia mara baada ya kufunga goli la kwamza

Young Africans Sports Club ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo, wameichapa timu ya Polisi Morogoro mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, mchezo uliofanyika leo katika Uwanja wa Taifa.

Vijana wa Jangwani wanaonolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts, wamefikisha jumla ya point 17 ikiwa ni pomiti 1 nyuma ya Azam Fc na point mbili nyuma ya Simba SC ambao wanaongoza ligi kwa point 1.

Yanga ilianza mbio za kusaka point 3 muhimu na katika sekunde ya 15 ya mchezo, Mshambuliaji Saimon Msuva alikosa bao la wazi baada ya kupewa pasarunanzuri na Haruna Niyonzima, lakini Msuva aligongana na mlinda mlango wa timu ya Polisi na kufanya atibiwe kwa dakika kadhaa.

Dakika ya 4 ya mchezo, Saimon Msuva aliipatia Yanga bao lwa kwanza baada ya kumalizia vizuri ya mwisho aliyopewa na Jeryson Tegete na mara hii Msuva hakufaya ajizi na kuukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao lake la pili katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Didier Kavumbagu aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 6 ya mchezo baada ya pasi nzuri za migongeo ya Haruna Niyonzima kumkuta Didier aliyewatoka walinzi wa Polisi na kuwazidi ujanja na kuipatia Yanga bao la pili.

Huku wachezaji wake wakionekana wanahitaji ushindi katika mchezo huo, Jeryson Tegete na Saimon Msuva walikosa mabao ya wazi katika ya 20 na dakika ya 25 hali iliyopelekea washabiki kupiga kelele kutokana na mchezo walivyokua wametawala.

Haruna Niyonzima alikosa kuipatia timu yake bao la tatu, baada kukosa penati iliyopatikana baada ya mlinzi wa Polisi Salmin Kis kumuangusha Msuva katika eneo la hatari na mwamuzi Alex Mahagi kuamuru penati iliyopigwa na Niyonzima ambaye mpira wake uligonga mlingoti na kutoka.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 2-0 Polisi Morogoro.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kuwaningiza Hamis Kiiza na Nurdin Bakari kuchukua nafasi za Haruna Niyonzima na Jeryson Tegete.

Mabadiliko hayo yalileta uhai kwa vijana wa Jangwani kwani katika dakika ya 58, Hamis Kiiza aliipati Yanga bao la 3 kufuaia kumalizia krosi nzuri ya David Luhende aliyewasumbua sana walinzi wa tim uya Polisi.

Kama washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini wangeweza kufunga mabao mengi zaidi, lakini umakini wao katika umaliziaji uliwafanya wasiweze kupata mabao mengine ya ziada.

Mpaka dakika 90 za mchezo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Yanga itasifiri kesho asubuhi kuelekea jijini Arusha tayari kwa mchezo wake dhidi ya timu ya JKT Oljoro mchezo utakaofanyika siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Sheikh Amei Abed.

Yanga: 1.Ally Mustapha, 2.Shadrack Nsajigwa, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub, 5.Mbuyu Twite, 6.Athuman Idd, 7.Saimon Msuva, 8.Haruna Niyonzima/Nurdin Bakari, 9.Didier Kavumbagu, 10.Jeryson Tegete/Hamis Kiiza, 11.David Luhende/Nizar Khlfan

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...