MASHADA INC

Tuesday, September 4, 2012

EXCLUSIVE: LIGI KUU MSIMU UJAO KUONYESHWA NA SUPERSPORT


Mwanga wa neema unazidi kuimulika ligi kuu ya Tanzania bara, baada ya kusaini mkataba mpya mzuri na Vodacom, ligi hiyo inaelekea kupata udhamini kutoka kwa kituo cha kurusha matangazo ya mpira cha Afrika kusini Supersport.

Ili kuweza kupata udhamini huo kumeandaliwa kipindi cha majaribio ya kurusha baadhi ya mechi za ligi msimu huu kupitia Supersport - ambacho kimepewa jina la "Supersport week in Tanzania".

Supersport kupitia majaribio hayo wataonyesha mechi zifuatazo: Azam vs JKT Ruvu tarehe 28 mwezi huu, Simba vs Tanzania Prisons tarehe 29/9, African Lyon vs Yanga tarehe 30/9, na mechi watani wa jadi Simba vs Yanga ya tarehe 3/10 - mechi hizi zote zitaonyeshwa live huku mechi ya mwisho ya Mtibwa na Ruvu itakuwa imerekodiwa.

Baada ya majaribio hayo kuna asilimia kubwa ligi kuu ya msimu ujao wa 2013/14 ikaanza kuonyeshwa na kituo hicho maarufu barani Afrika.

SOURCE; http://www.shaffihdauda.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...