Friday, February 8, 2013

D'BANJ, MICASA MUSIC NA MUTHONI WA KENYA KUTUMBUIZA KWENYE FAINALI YA AFCON 2013


Michuano ya wiki tatu ya kombe la mataifa ya Afrika, Orange AFCON, inayoendelea nchini Afrika Kusini inatarajia kumalizika Jumapili hii kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo mjini Johannesburg.

Wasanii sita wa Afrika wametajwa kutumbuiza kwenye fainali hizo ambao ni pamoja na staa wa Nigeria D’Banj, Zonke, Kelly Khumalo, Thembesile Ntaka wa Afrika Kusini, Muthoni wa Kenya na kundi la Micasa Music.

Sherehe hizo za ufungwaji wa michuano ya AFCON zitachukua nusu saa ambapo zitatanguliwa na presentation na performance ya Yvonne Chaka Chaka akiwa kama balozi mwema wa Roll Back Malaria Partnership. Atasindizikizwa na mchezaji wa zamani Mark Fish atakayetoa hotuba fupi kuhusu Malaria.

Nigeria na Burkina Faso zitakutana kwenye fainali ya michuano hiyo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...