Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA amemtaka raisi Kikwete authibitishie umma wa Watanzania ni kwa namna ipi CHADEMA wanawadanganya watanzania hii imetokana na Kauli ya Mwenyekiti huyo wa CCM kutamka kwamba CHADEMA wanaudanganya umma SUGU amehoji bungeni je Kusema ukweli ni kuupotosha Umma..!? Hii hapa ndio kauli ya Mh JOSEPH MBILINYI
"...kikwete katuita chadema waongo..hivi sisi na ccm akiwemo
yeye nani muongo kwenye hili taifa? na uongo wetu ni kuhusu nini??!! EPA?! RICHMOND na DOWANS? au tuliposema bungeni kwamba serikali ya ccm(...chini ya Kinana) inauza TWIGA na FARU wetu nje ya nchi?! na au kuhusu zaidi ya bilioni 300 ambazo maofisa wa serikali yake wameficha USWIZI etc etc etc???!!! ni vizuri kikwete angesema kama haya yote ni uongo kabla MH hajaupotosha umma kwa kusema CHADEMA na Dr Slaa(tena kwa kumtaja kwa jina) ni waongo..."
Mh. Joseph Mbilinyi
No comments:
Post a Comment