Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwandishi wa habari wa Clouds FM msanii wa filamu Elizabeth Michael hajatoka nnje kwa dhamana bali kesi yake iliyosikilizwa leo kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam itahamishiwa kwenye mahakama kuu ya Tanzania.
Hivyo ni kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na hivyo jalada la kesi ya LULU limefunguliwa rasmi leo katika mahakama hiyo.
Awali kulikua na taarifa mbalimbali mtandaoni nchini kuwa mahakama imemwachia kwa dhamana mwigizaji huyo anaekabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya mwigizaji Steven Kanumba.
Kutokana na maamuzi ya Leo Lulu ataendelea kubaki gerezani Segerea mpaka mahakama kuu itakapopanga siku ya kuanza kusikiliza kesi hiyo.
Leo mashahidi zaidi ya sita wametoa ushahidi wao mahakamani hapo akiwemo yeye mwenyewe LULU aliyesimulia jinsi tukio hilo lilivyokuwa.
TUNAOMBA RADHI KWA TARIFA ILIYOTOKA HAPO MWANZO KUWA LULU KATOKA KWA DHAMANA.
No comments:
Post a Comment