Tuesday, November 22, 2011

HATARI; IJUE KIMBOKA DUKA LA WAREMBO.

NILIPO AMBIWA NILIKATAA MPAKA NILIPOONA KWA MACHO YANGU SI UNAJUA HABARI YA KUAMBIWA LAZIMA IMEONGEZWA AU KUPUNGUZWA NENO!

KIMBOKA ni eneo maarufu sana kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam hasa vijana. Eneo hilo lipo Buguruni sheli mkabala na kituo cha magari yaendayo gongo la mboto, Eneo ambalo limefanywa duka la warembo, ukipita mchana huwezi kutegemea kama eneo hilo kuna ufuska kiasi hicho.Nilishindwa kuamini nikionacho pale nilipokuta kundi kubwa la watoto,akina dada na akina mama pia wakiwa wamevaa nusu uchi wakifanya ukahaba nje ya baa maarufu ijulikanayo kama KIMBOKA.
Nilianza kazi yangu kwa kufanya mahojiano na mmoja wa vijana waliokua wengi katika eneo hilo ambae hakupenda jina lake litajwe. Kijana huiyo alieleza bayana kuwa yeye ni mme wa mmoja wa wanawake wanaojiuza na yeye yuko pale kama mhasibu kwani anamtizama mke wake kila akipata mteja yeye ndio nanachukua na kuweka pesa...Aliendelea na kusema kuwa wrembo walio wengi wako na wapenzi,mabwana au wachumba zao ambao pia wanafanya kazi ya kushika pesa za wapenzi wao wanaouza miili yao!!!!!! Akizungumza na UJIO WANGU kijana huyo anasema yeye na mkewe walikubaliana kufanya hivyo kutokana na ugum wa maisha kwani wote hawana elimu na hawana njia yeyote ya kuwafanya waishi japo maisha ya kawaida kwani wanahitaji kula, mavazi, kulipa kodi ya nyumba n.k.
SUALA LA UKAHABA LINAZIDI KUKUA KWA KASI HUKU SERIKALI IKIWA IMELIFUMBIA MACHO SUALA HILI. NI VEMA JUHUDI ZA KUPINGANA NA UKIMWI ZIKAANZIA KATIKA JAMBO HILI KWANI UKUAJI WAKE UNATISHA!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...