Wednesday, November 23, 2011

UHAI CUP: AZAM B WAIADABISHA SERENGETI BOYS

SAIMON MSUVA-mfungaji wa magoli yote matatu akiwa amekabidhiwa mpira.
Timu ya soka ya Azam B(U20) inayofundishwa na IDD CHECHE leo jioni imeiadhibu timu ya taifa U20 SERENGETI BOYS kwa  jumla ya magoli matatu,SAIMON MSUVA aliyefuga magoli mawili kipindi cha kwanza na kufunga idadi katika kipindi cha pili kwa kupachika goli la tatu na kuondoka na mpira wake!

Kwa ushindi huo Azam wametinga fainali itakayochezwa ijumaa dhidi ya Simba majira ya saa tisa jioni, kabla ya mchezo wa fainali saa tatu asubuhi utachezwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.Akizungumza na UJIO WANGU kocha wa azam ameiomba TFF kuzingatia sheria kwani katika ligi hiyo kumekua na ukiukwaji mkubwa wa sheria hasa udanganyifu katika umri. Nao mashabiki wametoa lawama zao kwa mabaunsa kuwa wanadai pesa ili kuruhusu kuingia uwanjani kinyume na utaratibu uliotangazwa kuwa hakuna kiingilio.

IDD CHECHE-Kocha wa Azam B
mchezaji wa serengeti boys

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...