Monday, December 19, 2011

MWANAFUNZI WA MIAKA 12 AKUTWA AKIJIUZA.

KIMBOKA! KIMBOKA!! Naamini hili halitakua jina geni sana maskioni mwa wapenzi wa blog hii kwani                                               wiki kadhaa zilizopita tulizungumzia eneo hili marufu kwa ukahaba hapa jijini  kwa sasa.
Katika tukio la aibu na la kusikitisha mama mmoja mwenyeji wa Vingunguti jijini hapa alijikuta akimwaga machozi baada ya kumkuta mwanae (12) akifanya ukahaba katika eneo hilo, mtoto huyo aliyimua mbio mara baada ya kumuona mama yake mzazi na kumwacha mama akiangua kilio.
Huyu ni mmoja kati ya wanao jiuza kimboka

Akizungumza na UJIO WANGU mama huyo anasema "nilikua naambiwa na majirani lakini nilipuuza kwa kudhani wanachuki na mwanangu na nilianza kuwachukia ila leo jirani yangu mmoja kanifuata na kuniambia nimfuate ili anithibitishie wanayosema kila siku kufika hapa ndio nimejionea mwenyewe" aliendelea kwa kusema mwanae anasoma darasa la sita(6) na ameumizwa sana na tabia ya mwanae kwani mtoto huyo hakuna anachokosa nyumbani.

Mama huyo alisema kuwa yeye anafanya kazi ya ulinzi katika kampuni moja hapa hapa jijini mara nyingi huwa anaingia kazini usiku na kumuacha mwanae peke yake nyumbani kwani haishi na baba wa mtoto.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...