Thursday, December 22, 2011

MAAFA MAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM.

Maji yalivyo jaa katika makazi ya watu
Wakazi wa Tandale jijini Dae es salaam wakisaidiana
kuvuka maji katika makazi yao
 Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha jijini Dar es salaam zinaendelea kuleta madhara makubwa hasa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni kama vile Jangwani, Tandale, Vingunguti-spenko,ulongoni-Gongo la mboto
na sehemu mbalimbali za jiji.
Mbali na kuharibu makazi ya watu mvua hizo zimesababisha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wadogo, pia mvua imeleta madhara makubwa katika sekta ya usafiri kwani barabara nyingi zimeharibika. Wananchi wengi wamekosa makazi na wangi wao wakipata hifadhi kwa ndugu zao,jamaa na marafiki huku waliokosa makazi wakiwa katika maeneo maalum yaliyotengwa na serikali kama vile Uwanja wa Taifa na sehemu mbalimbali yamejengwa mahema!


Hapa ni Jangwani katika makazi ya watu
Barabara nyingi hazipitiki.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...